Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akizungumza mara baada ya kipindi cha Maswali na Majibu kumalizika katika kikao cha Tano bunge la 15 leo tarehe 8 April 2019 Bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Vijana, Kazi Ajira na Wenyeulemavu Jenista Mhagama akifafanua jambo wakati wa kikao cha Tano cha Bunge la 15 kabla ya wabunge kuendelea kuchangia hoja Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu leo tarehe 8 April 2019 Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.

Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza Mhe. Andrew Chenge akijibu miongozo ya wabunge wakati wa kikao cha Tano cha Bunge la 15 kabla ya wabunge kuendelea kuchangia hoja Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mkutano wa 15 wa Bunge kikao cha tano leo tarehe 8 April 2019 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Januari Makamba akifafanua jambo wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu katika Mkutano wa 15 wa Bunge kikao cha tano leo tarehe 8 April 2019 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula akifafanua jambo wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu katika Mkutano wa 15 wa Bunge kikao cha tan oleo tarehe 8 April 2019 jijini Dodoma.

Mbunge wa Babati Mjini Mhe. Paulina Gekuli akichangia hoja wakati wa majadiliano kuchangia hoja Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika Mkutano wa 15 wa Bunge kikao cha tano leo tarehe 8 April 2019 jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angellah Kairuki wakati wa Mkutano wa 15 wa Bunge kikao cha tan oleo tarehe 8 April 2019 jijini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Madini, Doto Biteko.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo wakifuatilia shughuli za Bunge wakati wa Mkutano wa 15 wa Bunge kikao cha tan oleo tarehe 8 April 2019 jijini Dodoma. ( Picha na: Frank Shija – MAELEZO)

292 thoughts on “Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *