Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akijibu swali la nyongeza toka kwa Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto(hayupo pichani) kuhusu maandalizi ya Timu ya Taifa ya Vijana wakati wa Kikao cha Bunge leo Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Hazzan Zungu akitoa matangazo alipokuwa akihitimisha kipindi cha maswali na majibu Bunge leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akijibu swali la Mhe. Sabreena Sungura (Mbunge wa Viti Maalum) hayupo pichani wakati wa Kikao cha Bunge leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akijibu swali wakati wa Kikao cha Bunge leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akijibu swali wakati wa Kikao cha Bunge leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangallah na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (katikati) wakati wa Kikao cha Bunge leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwezeshaji, Mhe. Angellah Kairuki akimsikiliza kwa makini Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (kulia) wakati wa Kikao cha Bunge leo Jijini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko. (Picha na MAELEZO)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail