Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Waziri wa Utalii na Maliasili, Dkt. Hamisi Kigwangalla, akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini mheshimiwa Emmanuel Mwakasaka, kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mheshimiwa Ummy Mwalimu leo bungeni. Waziri Kigwangala amejibu maswali ya wabunge kwa mara ya kwanza baada ya kutokuwepo bungeni kwa muda wa miezi mtatu kutokana na kupata ajali eneo la Magugu mkoani Arusha mwezi Agosti mwaka huu.

Mbunge wa Mtama, mheshimiwa Nape Nnauye akibadilishana mawazo na mbunge wa Kigoma Mjini, mheshimiwa Zitto Kabwe wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa kumi na tatu wa Bunge wa Jamhuri la Muungano wa Tanzania kinachoendelea jijini Dodoma leo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Isidor Mpango na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji, wakifuatilia kwa makini hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, akibadilishana mawazo na Mbunge wa Kigoma Mjini, mheshimiwa Zitto Kabwe wakati wa kikao cha Bunge kinachoendelea jijini Dodoma.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail