Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani Mhe. Zaynabu Matitu (hayupo pichani) kuhusu changamoto za usikivu wa TBC wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi akijibu swali wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Josephat Kwandikwa akijibu swali wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angellina Mabula akijibu swali wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 07 Novemba 2018 jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Jenista Mhagama wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 07 Novemba 2018 jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana, Anthony Mavunde.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu Jenista Mhagama wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija)

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail