Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akifanya majumuisho wakati wa kuhitimisha hoja ya Mapendekezo ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2018/19 leo Bunge Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akiwasilisha majibu ya hoja za baadhi ya wabunge wakati wa kuhitimisha hoja ya Mapendekezo ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2018/19 leo Bunge Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akifafanua jambo wakati wa kuhitimisha hoja ya Mapendekezo ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 leo Bunge Jijini Dodoma.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akifafanua jambo wakati wa kuhitimisha hoja ya Mapendekezo ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 leo Bunge Jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo wakati wa kuhitimisha hoja ya Mapendekezo ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 leo Bunge Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiteta jambo na Mbunge wa Viti Maalum (Vijana), Halima Bulembo katika kikao cha kuhitimisha hoja ya Mapendekezo ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 leo Bunge Jijini Dodoma.

Bibi. Bahati Ramadhani akiwa amembeba mume wake Bw. Jivunie Mbunda ambaye ni mlemavu walipotambulishwa bungeni leo Jijini Dodoma. Wanandoa wamefunga ndoa ya aina yake hivi karibuni , pia bunge limeazimia kuwachangia shilingi elfu ishirini kutoka katika posho ya kila mbunge leo Jijini Dodoma. (Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma)

77 thoughts on “Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *