Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio katika picha Bungeni Leo

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu Bungeni leo Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akimsikiliza Mbunge wa Songea Mjini Mhe Dkt  Damas Ndumbaro wakati wa kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya Nishati wakati wa kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe wakati wa kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.

 

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage akionyesha kitabu chenye idadi ya Viwanda vyote nchini wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019.Kitabu hicho kina kurasa mia tisa.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Sumve Mhe.Richard Ndassa  wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)  walipomtembelea leo Bungeni.

 

 

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe akimskiliza Mbunge wa Sumve Mhe.Richard Ndassa Bungeni leo Jijini Dar es Salaam.

 

146 thoughts on “Matukio katika picha Bungeni Leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *