Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio katika Picha Bungeni

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akitolea ufafanuzi maswali mbalimbali ya wabunge leo Jijini Dodoma.

Wabunge wa Viti Maalum Mhe.Munira Mustafa Khatib na Mhe.Halima Abdallah Bulembo wakifurahia jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso akijibu swali wakati wa kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.

Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Mwambalaswa akiuliza swali wakati wa kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.William Ole Nasha wakati wa  kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk Augustine Mahiga akizungumza jambo na  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Hamisi Kigwangalla na Naibu wake Mhe.Japhet Hasunga  wakati wa  kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail