Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio katika Picha Bungeni

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akiongoza kikao cha thelathini na tatu cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.

Viongozi waandamizi wa Wizara ya maliasili na Utalii wakiongozwa na Katibu mkuu Meja Jenerali  Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu Dkt.Aloyce Nzuki wakifatilia shughuli mbalimbali za Bunge leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri-TAMISEMI Mhe.Josephat Kandege akijibu hoja mbalimbali za wabunge  wakati kikao cha thelathini na tatu cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt Hamisi Kigwangalla  akiteta jambo na Naibu wake Mhe.Japhet Hasunga wakati kikao cha thelathini na tatu cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt Hamisi Kigwangalla akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt Suzan Kolimba  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati kikao cha thelathini na tatu cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.

59 thoughts on “Matukio katika Picha Bungeni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *