Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Awamu ya Pili ya Mafunzo Kwa Waandishi wa Habari za SADC

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo, Brigedi ya Magharibi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Wilbert A. Ibuge akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo kwa kundi la pili la waandishi hao.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo .

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari- MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo kwa waandishi hao.

Katibu Mkuu mstaafu Balozi Hebert Mrango akisisitiza jambo wakati wa mafunzo kwa kundi la pili la waandishi wa habari wanaojengewa uwezo ili waweze wa kuandika na kuripoti habari za nchi wanachama wa SADC, hayo yamejiri mjini Morogoro Julai 12, 2019 ambapo mafunzo ya kundi la pili kwa waandishi hao yanafanyika kwa siku tatu.

Katibu Mkuu mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mussa Uledi akijibu hoja mbalimbali za waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuandika na kuripoti habari za SADC kwa weledi Bw. Henry Mabumo akieleza jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika na Jumuiya hiyo kupitia fursa zilizopo katika nchi wanachama, hayo yamejiri leo Julai 12, 2019 mjini Morogoro wakati wa siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi hao.

(Picha zote na Abukari Kafumba)

7 thoughts on “Matukio Katika Picha Awamu ya Pili ya Mafunzo Kwa Waandishi wa Habari za SADC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama