Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Bungeni Leo.

. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisisitiza jambo kwa wabunge kabla ya kuahirishwa kwa mkutano wa kumi nne wa Bunge la Kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (MB) akisisitiza kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi hapa nchini wakati wa mjadala kuhusu muswaada wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali leo Bungeni Jijini Dodoma.

Mbunge wa Kuteuliwa Bi Anne Kilango Malechela akipongeza hatua ya Serikali kufuta kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye mchuzi wa zabibu ili kuwainua wakulima wa zao hilo hapa nchini.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani leo Bungeni Jijini Dodoma.

Baadhi ya Waheshimiwa Mawaziri wakiteta jambo na mwanasheria mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi leo Bungeni Jijini Dodoma kabla ya kuahirishwa kwa mkutano wa kumi nne wa Bunge la Kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma


FacebooktwittermailFacebooktwittermail