Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Bungeni Leo.

Mwanasheria Mkuu Wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi akila kiapo cha uaminifu Bungeni mapema leo , Baada ya Kuteuliwa na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Kushika wadhifa huo hivi Karibuni. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt. Stephen Kagaigai akishuhudia kiapo hicho.

 

. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimpongeza Mwanasheria Mkuu Wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi mara baada ya kiapo cha uaminifu Bungeni mjini Dodoma, mapema leo .

. Mwanasheria Mkuu Wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi akisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.

 

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akisistiza jambo wakati wa Kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.

 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Walemavu) Mhe. Stella Ikupa ( wa kwanza kushoto) akitoa maelezo Bungeni kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa walemavu wa ngozi wanapata mafuta maalum yakujikinga na athari za mionzi ya jua.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nishati Dkt. Merdard Kalemani mapema leo Bungeni mjini Dodoma.

(Picha zote na  Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)

135 thoughts on “Matukio Bungeni Leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama