Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mashindano ya Uandishi wa Insha Kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira

Tanzania itaungana na Jumuiya ya Kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani tarehe 5 Juni, 2020. Katika maadhimisho ya mwaka huu, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau wa Mazingira imeandaa mashindano ya uandishi wa insha kuhusu masuala ya Mabadiliko ya tabianchi na mazingira.

Lengo ni kukuza uelewa na kuhamasisha ubunifu kwa wanafunzi na vijana katika masuala ya hifadhi ya mazingira pamoja na kubainisha uelewa wa kizazi cha sasa kuhusu sekta husika.

WALENGWA

Mashindano haya yanalenga kuhusisha wanafunzi katika ngazi ya shule za Msingi na Sekondari, Vyuo vya Elimu ya Juu hapa nchini.

MADA

Shule za Msingi:

Athari za mabadiliko ya Tabianchi nchini

Shule za Sekondari: 

Athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye ustawi wa Bioanuai (Kidato cha 1 hadi 4)

Athari za mabadiliko ya tabianchi kwa maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii (Kidato cha 5 hadi 6)

Vyuo Vikuu na vya Kati

Mikakati ya kitaifa na kimataifa ya kuhimili athari za Mabadiliko ya Tabianchi.

TATHMINI

Mawasilisho ya insha yatatathiminiwa kulingana na uhalisia na mifano ya maisha ya sasa, ubunifu na umahiri wa lugha iliyotumika katika maandiko (kingereza au kiswahili).

UREFU WA INSHA

 • Kwa Shule za Msingi, insha isizidi maneno mia tano (500)
 • Kwa Shule za Sekondari, insha isizidi maneno elfu moja (1000)
 • Kwa Vyuo vya Elimu ya Juu, Insha isizidi maneno elfu mbili (2000)

MUDA WA KUWASILISHA INSHA

Mwisho wa kupokea insha itakuwa tarehe 10 Juni, 2020.

Insha zitumwe kwa njia ya Email martha.ngalowera@vpo.go.tz au enock.sanga@vpo.go.tz watakaoandika kwa kalamu wascan karatasi husika na kutuma kwa njia ya email mojawapo iliyoainishwa hapo juu.

UTAMBULISHO

Muhusika aandike Jina kamili, shule/Chuo anachosoma, namba ya usajili wa shule /Chuo, Darasa/Kidato /mwaka wa chuo ambao muhusika yupo chuoni.

ZAWADI ZITAKAZOTOLEWA KWA WASHINDI ni pamoja na compyuta mpakato, Cheti cha ushindi, Begi na vifaa vya shule chupa ya kuwekea maji, na fulana na kofia. Kwa kila shule anayotoka mshindi watapata Mipira miwili pamoja na  vifaa vya kufundishia.

HAFLA YA KUTOA ZAWADI

Zawadi kwa washindi zitatolewa tarehe 17 Juni, 2020 siku ya Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame Duniani.

MAWASILIANO

Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali wasiliana na Bw. Enock Sanga kupitia simu namba 0753 326 234 au Bi. Martha Ngalowera namba 0784589610. Pia tembelea tovuti yetu ya www.vpo.go.tz, www.daressalaam.diplo.de, www.panda.org na www.tanzania.un.org

ANGALIZO: Wafanyakazi wa taasisi zilizoandaa shindano hili pamoja na ndugu zao hawaruhusiwi kishiriki.

Tangazo hili limetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na WWF, GIZ, Ubalozi wa Ujerumani na Vodacom Foundation)

 

 

 

 

6 thoughts on “Mashindano ya Uandishi wa Insha Kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira

 • July 18, 2020 at 7:04 am
  Permalink

  Hongereni kwa kazi nzuri hapo wizarani
  Naitwa mwalim mtega wa mkwawa sekondari. Shule yetu ni miongoni mwa washiriki wazuri wa mashindano ya uandishi wa insha. tunasikitika hatukupata taarifa hii ya mashindano ya uandishi wa insha juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi kutokana na athari za uharibifu wa mazingira. Next time tupo PAMOJA

  Reply
 • August 10, 2020 at 2:58 am
  Permalink

  Hi there, I wish for to subscribe for this weblog to take
  most recent updates, therefore where can i do it please help.

  Reply
 • August 14, 2020 at 5:59 am
  Permalink

  I am really delighted to glance at this web site posts which consists of plenty
  of helpful facts, thanks for providing such statistics.

  Reply
 • August 24, 2020 at 3:35 pm
  Permalink

  I’m really enjoying the design and layout of your blog.
  It’s a very easy on the eyes which makes it much more enjoyable for
  me to come here and visit more often. Did you hire out a developer
  to create your theme? Exceptional work! 31muvXS cheap flights

  Reply
 • August 26, 2020 at 9:24 pm
  Permalink

  I am actually happy to read this website posts which
  includes tons of useful data, thanks for providing these kinds of data.

  Reply
 • August 31, 2020 at 2:15 am
  Permalink

  What’s up to every , since I am truly keen of reading this web site’s post to be updated regularly.
  It contains good information.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama