Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Maonesho ya Wiki ya Sheria Yaanza Rasmi.

Mkurugenzi wa Malalamiko na Maadili – Mahakama ya Tanzania, Mhe. Happiness Ndesamburo akisikiliza malalamiko ya mmoja wa wananchi aliyetembelea katika Banda hilo lililopo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Watumishi wa Mahakama wakiendelea kuwasikiliza Wananchi waliotembelea katika maonesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na nchi nzima kuanzia Januari 27 – 31, 2018, kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ni Februari 01, 2018 kitaifa itafanyika jijini Dar es Salaam na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Elimu ya Sheria ikiendelea kutolewa kwa wananchi waliotembelea viwanjani hapo mapema Januari 27, 2018 siku ambayo Maonesho yameanza rasmi. Elimu ya Sheria inaendelea nchi nzima pia kwa upande wa Dar es Salaam, huduma hii inatolewa katika vituo mbalimbali vikiwemo vya Sinza, Magomeni, Mbezi Mwisho, Kawe Stendi, Tegeta, Bunju, Mbagala Zakiem, Keko, Mjimwema, Tandika, Mombasa, Kitunda, Banana, Segerea, Ilala sokoni, Kariakoo, Buguruni Sheli na Gerezani.

Muonekano wa sehemu ya Mabanda ya Watoa huduma ya Sheria pamoja na wananchi walipotembelea kupata huduma.

Muonekano wa Banda la Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika Maonesho ya Wiki ya Sheria nchini, yanayoendelea nchi nzima, Wizara ni Moja ya Taasisi za Sheria zinazoshiriki katika Maonesho hayo, Taasisi nyingine ni: Tume Ya Utumishi Wa Mahakama, Ofisi Ya Mwanasheria Mkuu Wa Serikali (Agc), Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP), Mkemia Mkuu Wa Serikali, TAKUKURU (PCCB), Wakala Wa Usajili, Ufilisi Na Udhamini (Rita) na nyingine nyingi.

3 thoughts on “Maonesho ya Wiki ya Sheria Yaanza Rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama