Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Manyara Waahidi Kuongeza Ufanisi Usimamizi Sekta ya Filamu

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo akizungumza katika mkutano baina yake na wajumbe wa Bodi za Filamu katika Mkoa wa Manyara uliofanyika mjini Babati mkoani Manyara jana. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo ngazi ya wilaya Bw. Cade Mshamu na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mweneyekiti wa Bodi hiyo ngazi ya Mkoa, Missaile Raymond Musa. Mkutano huo ulilenga kuwajengea uwezo wajumbe wa bodi hizo juu ya majukumu yao na uelewa kuhusu kanuni na sheria ya filamu

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya katika mkutano baina yake na wajumbe wa bodi hizo kutoka Mkoa wa Manyara jana mjini Babati. Mkutano huo ulilenga kuwajengea uwezo wajumbe wa bodi hizo juu ya majukumu yao na uelewa kuhusu kanuni na sheria ya filamu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu ngazi ya mkoa, Bw. Missaile Raymond Musa akizungumza katika mkutano baina Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo (kulia) na wajumbe wa Bodi za Filamu za Mkoa wa Manyara uliofanyika mjini Babati jana. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo ngazi ya wilaya Bw. Cade Mshamu.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo ngazi ya wilaya Bw. Cade Mshamu akizungumza katika mkutano baina Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo (kulia) na wajumbe wa Bodi za Filamu za Mkoa wa Manyara uliofanyika mjini Babati jana. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu ngazi ya mkoa, Bw. Missaile Raymond Musa.

Baadhi ya wjumbe wa Bodi za Filamu katika Mkoa wa Manyara wakifuatilia mada kuhusu wajibu na majukumu ya bodi hizo kutoka kwa Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo (hayupo pichani) jana mjini Babati.

Mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Filamu ya Mkoa wa Manyara Bi. Anna Fissoo ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa akichangia mada wakati wa mkutano baina ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo (hayupo pichani) na wajumbe wa bodi hizo uliofanyika mjini Babati jana.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi za Filamu za Mkoa na Wilaya mkoani Manyara mara baada ya kumaliza mkutano jana mjini Babati. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO, Babati, Manyara)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail