Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mama Samia: Michezo ni Mwanzo Mzuri wa Kupambana na Saratani ya Shingo ya Kizazi

Mgeni Rasmi wa mashindano ya NBC Dodoma Marathon ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake wakati wa kuhitimisha mashindano hayo yaliyofanyika leo Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma na kushirikisha wanariadha kutoka hapa nchini na  nchi za Kenya, Malawi na Uganda ambapo  washiriki elfu 3000 wameshiri.

Na Eleuteri Mangi, WHUSM-Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan amewataka wanawake nchini kujitokeza kupima afya zao mapema ili kujua hali zao hatua inayosaidia kupambana na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.

Mama Samia amesema akiongea wanamichezo walioshiriki mbio za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Dodoma Marathon yaliyofanyika leo Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma.

“Akinamama mjitokeze kupima afya zenu mapema, msiogope kwenda kupima saratani ya mlango wa kizazi hatua inayosaidia kupambana na saratani hii na kulinda afya za watu wetu” amesema Mama Samia.
Mgeni Rasmi wa mashindano ya NBC Dodoma Marathon ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake wakati wa kuhitimisha mashindano hayo yaliyofanyika leo Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma na kushirikisha wanariadha kutoka hapa nchini na  nchi za Kenya, Malawi na Uganda ambapo  washiriki elfu 3000 wameshiri.

Katika mashindano hayo, Makamu wa Rais Mama Samia amewapongeza wanawake kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mbio hizo  hatua inayoonesha ni mwanzo mzuri wa kupambana na saratani ya shingo ya kizazi nchini.

Aidha, Makamu wa Rais Mama Samia amesema mashindano ya NBC Dodoma Marathon yamekuja muda mwafaka hatua inayosaidia wanamichezo kujiandaa vema katika mashindano ya Olimpik yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni 2021 Tokyo nchini Japan pamoja na kuchangisha kiasi cha takriban zaidi ya Sh. milioni 75 ambazo zimeelekezwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar kusaidia mapano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais Mama Samia amesema kuwa Serikali ipo mstari wa mbele katika kukuza sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo kama alivyoahidi Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kufungua Bunge la 12 hivi karibuni Jijini Dodoma.

2 thoughts on “Mama Samia: Michezo ni Mwanzo Mzuri wa Kupambana na Saratani ya Shingo ya Kizazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *