Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mama Magufuli Atoa Futari kwa Ajili ya Familia Zenye Uhitaji Jijini Dar Es Salaam Leo

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akiongea machache wakati wa hafla ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, amewasihi Waislamu nchini kuendelea kuliombea Taifa muda wote, hususan katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuendeleza mshikamano bila kujali dini ama kabila tabaka zao.

Mama Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 22 Mei, 2019 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.

Vyakula alivyotoa ni tani 5 za mchele, tani 3 za sukari na tende.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile na wawakilishi wa vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimsiliza Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Muma akitoa shukurani wakati wa kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019

Mama Magufuli pia amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, azikubali funga za Waislamu wote na kuwalipa malipo stahiki wakati wakitekeleza moja ya nguzo muhimu za Dini ya Kiislamu.

“Kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kipindi cha toba, ni kipindi cha kutenda matendo mema na kujizuia na vitendo viovu” amesema Mama Magufuli.

Mama Magufuli amesema licha ya kwamba Tanzania ina watu wa imani za dini tofauti lakini siku zote wananchi wake wamekuwa wakishirikiana nyakati za dhiki na za raha bila ubaguzi.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Muma msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 019

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi Mkurugenzi wa Hija wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile pamoja na wawakilishi wa vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji baada ya hafla ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.

Ametoa mfano kuwa licha ya tofauti za kidini zipo baadhi ya familia ambazo Baba Muislamu na Mama ni Mkristo zinaishi kwa amani na kushirikiana katika masuala yote ya kifamilia na kwamba sifa hii ni moja nguzo muhimu za umoja wa Watanzania.

“Binafsi nakumbuka zamani nikiwa mdogo tulikuwa tunatafuta Muislamu aje atuchinjie kuku ama mbuzi ama ng’ombe”, alisema na kuongezea: “Ni kutokana na utamaduni huo uliojengeka miongoni mwa Watanzania, leo nimeguswa kutoa sadaka yangu kwa ajili ya ndugu zangu wenye uhitaji.”

 

9 thoughts on “Mama Magufuli Atoa Futari kwa Ajili ya Familia Zenye Uhitaji Jijini Dar Es Salaam Leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama