Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Makamu Wa Rais Mhe. Samia Amuwakilisha Rais Magufuli Kuhudhuria Kuapishwa Rais Mpya wa Botswana

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Edgar Lungu wa Zambia kwenye Hafla ya kuapishwa Rais Mpya wa Botswana Dkt. Mokgweetsi E. K. Masisi iliyofanyika leo Novemba 01, 2019 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Botswana Indoor Arena Jijini Gaborone Botswana.

Rais Mpya wa Botswana Dkt. Mokgweetsi E. K. Masisi akihutubia Viongozi wa Nchi mbalimbali na Wananchi wa Botswana Baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo leo Novemba 01,2019 kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Botswana Indoor Arena Jijini Gaborone Botswana.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Edgar Lungu wa Zambia na Rais Emmason Mnangagwa wa Zimbabwe wakishuhudia wakati Rais Mpya wa Botswana Dkt. Mokgweetsi E. K. Masisi alipokuwa akila kiapo kuiongoza Nchi hiyo leo Novemba 01,2019 kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Botswana Indoor Arena Jijini Gaborone Botswana

53 thoughts on “Makamu Wa Rais Mhe. Samia Amuwakilisha Rais Magufuli Kuhudhuria Kuapishwa Rais Mpya wa Botswana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *