Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Makamu wa Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan Mgeni rasmi mashindano ya NBC Marathon


Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo  kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Suyuph Singo akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu mashindano ya NBC  Marathon yatakayofanyika Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Kushoto ni Meneja Mahusiano na Serikali wa Benki ya NBC Bw. William Kallaghe.

Na Eleuteri Mangi, WHUSM-Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika mashindano ya NBC Marathon yatakayofanyika Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma ambapo pia atashiri mbio za Kilomita 5.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Suyuph Singo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo leo Novemba 21, 2020 Jijini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kueleza  hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya mashindano hayo.

“Lengo la mashindano ya NBC Marathon ni kwa ajili ya kuchangisha fedha  kusaidia  mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kansa ya shingo ya kizazi katika hospitali ya Ocean Road ya jijini Dar es salaam” alisema Bw.Singo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *