Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Makamu wa Rais Azindua Wiki ya Huduma za Fedha Mwanza

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa watoaji wa huduma za kifedha nchini kutazama upya masharti ya mikopo, ikiwemo dhamana ya mali zisizohamishika kwa kuwa ni kikwazo kwa wajasiriamali pamoja na kutafuta njia za kibunifu katika kuwafikia vijana hapa nchini ili waweze kupata mikopo itakayoinua maisha yao na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 24 Novemba, 2022 wakati akifungua Maadhimisho ya Pili ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza. Aidha, amesema Riba ya mikopo ya wastani wa asilimia 16 bado ni mzigo kwa Watanzania walio wengi, hivyo amesisitiza kila benki kupitia umoja wao (TBA) kuchambua mizizi ya changamoto hiyo na kupunguza zaidi riba kwa wakopaji.

Halikadhalika, Makamu wa Rais ametoa wito kwa watoaji wa huduma za kifedha nchini kupunguza gharama za kutuma na kupokea pesa kimataifa kwa kuwa zimekua zikisababisha wageni pamoja na diaspora kutumia njia zisizo rasmi wanapowatumia pesa jamaa zao hapa nchini. Ameongeza kwamba kwa upande wa credit cards, tozo za benki na mawakala wao zimekuwa mzigo na hivyo kukwamisha watalii kununua vitu kwa wingi na kuikosesha mapato Serikali na watoa huduma mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama