Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Makamu wa Rais Awasili Nchini Uganda Kushiriki Mkutano wa Africa Now Summit 2019

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya ndege ya Air Tanzania aina ya Airbus A220-300 wakati akielekea nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa Africa Now Summit 2019 unaoanza kesho tarehe 12 mjini Kampala Uganda.

: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dkt. Aziz P. Mlima mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe nchini Uganda.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe. Philemon Mateke mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe tayari kwa kushiriki mkutano wa Africa Now Summit 2019 utakaofanyika mjini Kampala tarehe 12 na 13 mwezi Machi, 2019.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 

94 thoughts on “Makamu wa Rais Awasili Nchini Uganda Kushiriki Mkutano wa Africa Now Summit 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *