Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Makabidhiano ya Vyeti vya Shukrani

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy J. Mwakatage (kulia) akimkabidhi cheti cha shukrani “certificate of appreciation” Meneja Mkuu wa Dar es Salaam Yacht Club (DYC) Bw. Brian Fernandes (kushoto) kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Dar es Salaam Yacht Club Masaki Jijini Dar es Salaam mapema leo hii.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy J. Mwakatage (kulia) akimkabidhi cheti cha shukrani “certificate of appreciation” nahodha wa Tanzania Sea Rescue (TSR) Bw. Ally Saleh Kitobe aliyeiwakilisha kampuni yake kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Dar es Salaam Yacht Club Masaki Jijini Dar es Salaam mapema leo hii.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy J. Mwakatage (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni zilizopewa vyeti vya shukrani “Certificate of appreciation” kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Brian Fernandes (wa tatu kushoto) kutoka Dar es salaam Yacht Club (DYC), Ally Saleh Kitobe (wa pili kushoto) kutoka Tanzania Sea Rescue na Issa Lwamba (wa pili kulia) kutoka Dar es Salaam Independent School (DIS). Makabidhiano yaliyofanyika mapema leo hii katika viwanja vya Dar es Salaam Yacht Club Masaki Jijini Dar es Salaam.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail