Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

MAJALIWA: TAKUKURU Hakikisheni Watanzania Hawarubuniwi

*Ni katika kuchagua viongozi kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ihakikishe Watanzania hawarubuniwi ili watumie vizuri utashi wao wa kisiasa kuchagua viongozi bora.

“Sote tunatambua kuwa Oktoba, mwaka huu Taifa letu litaendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani… mna jukumu zito la kuhakikisha Watanzania hawarubuniwi na msimuonee au kumpendelea yeyote kwa maslahi yenu binafsi.”

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Agosti 12, 2020) alipofungua jengo la Intelijensia TAKUKURU Makao Makuu Dodoma.Amewasihi watumie vizuri ofisi hiyo kukusanya taarifa muhimu za kiintelijensia zinazowahusu wagombea, vyama au wananchi watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi mkuu.

Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 28, 2020 na kwamba wanawajibu wa kuchagua Serikali bora na kiongozi bora atakayewaletea maendelea maendeleo. “Chagueni kiongozi mwenye maono aliyetenda na atakayetenda.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *