Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Atembelea Kambi ya Wakimbizi ya Nduta Wilayani Kibondo

Kibao kinachoonesha ilipo Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo ambayo ilitembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Februari 18, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye moja ya madarasa katika Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa iliyopo kwenye Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019. Wapili kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua madaftari ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa wakati alipotembelea baadhi ya madarasa ya Shule hiyo, Februari 18, 2019. Wapili kushoto ni mkewe Mary.

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiteta na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019.

1382 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watoto wa Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa wakati alipokagua madarasa ya Shule hiyo katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail