Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Apokea Misaada kwa Ajili ya Mapambano Dhidi ya CORONA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. 4, 000,000,000/= kutoka kwa Meneja Mkazi (Country Manager) wa Kampuni ya Madini ya Barric – Twiga Minerals, Hilaire Diarra (kushoto) na Msaidizi wake, Neema Ndossi (kulia) ukiwa ni mchango wa Kampuni hiyo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID – 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020. Wa pili kushoto ni Waziri wa madini, Doto Biteko na wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. 1,000,000,000/= kutoka kwa Mfanyabiashara, Rostam Aziz (wa tatu kushoto) ukiwa ni mchango binafsi wa mfanyabiashara huyo wa kuunga mkono mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID – 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile,kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Makampuni ya Taifa, Abdulkarim Shah, wa pili ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Taifa Gas, Khamis Ramadhani na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Said Matamwe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea kutoka kwa wadau msaada wa fedha pamoja na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) wenye thamani ya sh. bilioni 6.226.

 

Baada ya kupokea kupokea msaada huo, Waziri Mkuu amewashukuru wadau hao kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya virusi vya corona, ambapo hadi sasa kesi 24 zimeripotiwa tangu kuanza kwa ugonjwa huo nchini na wagonjwa watano wamepona.

Waziri Mkuu amepokea msaada huo leo (Jumatano, Aprili 8, 2020) katika Ofisi Waziri Mkuu Mlimwa, jijini Dodoma. Amewataka Watanzania waendelee kushirikiana na Serikali katika kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea lita 50,000 za mafuta kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah ( wa pili Kushoto) na Meneja Uzalishaji wa kampuni hiyo, Lameck Hiliyai (kulia) ukiwa ni mchango wa Kampuni hiyo wa kuunga mono mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID -19 nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020. Wa tatu Kushoto ni Waziri wa Madini, Doto Biteko, Wa pili Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, ofisi ya Waziri Mkuu, Kanalı Said Matamwe.

Amesema hadi sasa jumla ya watu 396 wapo kwenye karatini katika maeneo mbalimbali yaliyotengwa wakiwemo wageni wanaoingia nchini ambao wanafuatiliwa afya zao na baada ya siku 14 kama watakuwa hawana maambukizi wataruhusiwa kuungana na familia zao.

 

Waziri Mkuu amesema Serikali kwa upande wake imeendelea kuchukua mbalimbali katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19 na kwa sasa imejiimarisha kwenye utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na virusi vya corona.

 

“Serikali inatoa misitizo kwa wananchi wazingatie maelekezo yanayotolewa kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka pamoja na kujiepusha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.”

 

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ili kuzuia usisambae kwa sababu hadi sasa mkoa huo unaongoza kwa kuwa na wagonjwa zaidi wa corona nchini.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau mbalimbali waliojitokeza kutoa michango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serkali za kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID – 19 kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma,

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuvishukuru vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano wanaoutoa katika kuelimisha umma namna ya kujikinga na virusi vya corona pamoja na wasanii waliotunga nyimbo za kuuelimisha umma namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

 

Miongoni mwa wadau waliotoa msaada huo ni kampuni ya Madini ya Twiga iliyotoa sh. bilioni nne, mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz ametoa sh. bilioni moja, kampuni ya Taifa Gesi imetoa sh. milioni 100 na kampuni ya mafuta ya Puma imetoa msaada wa mafuta lita 50,000 zitakazotumika katika magari yanayotoa huduma za kupambana na corona nchini yakiwemo magari ya kubebea wagonjwa.

 

Wengine ni kampuni ya TEHAMA ya Huawei imetoa vifaa kuendeshea mikutano kwa njia ya video ambavyo ni cloudlink camera tatu, Cloudlink Mic tatu, Cloudlink TV terminal tatu, Cloudlink Platform pamoja na Thermal Imaging Temperature Measuring System moja vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 940, Asasi za Kiraia (AZAKI) zimetoa sh. milioni 79.

 

Baada ya kupokea misaada hiyo, Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli aliwashukuru wadau hao kwa vitu mbalimbali walivyovitoa kwa ajili ya kupambana na COVID-19 kwani vifaa pamoja na fedha walizozitoa zitaisadia Serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo.

 

Kuhusu wadau wengine wanaohitaji kutoa misaada, Waziri Mkuu amesema ofisi yake iko wazi pia wanaweza kupeleka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwa walio nje ya nchi au sehemu yoyote wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti Na: 9921159801 yenye jina la National Relief Fund Electronic.

 

Awali, mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi alisema ametoa sh. bilioni moja ambayo ameielekeza katika kununua vitakasa mikono ambavyo vitatumiwa na wasafiri wa daladala wa Dar es Salaam na Zanzibar ili waweze kutumia kabla ya kupanda usafiri huo, hivyo kuweza kujikinga.

 

Pia, Mfanyabiashara huyo ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwaongoza Watanzania kwa hekima na busara na kuwaepusha na taharuki kama ilivyotokea katika mataifa mengine. Amempongeza Waziri Mkuu na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa namna wanavyoshiriki katika kukabiliana na corona.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

 1. L. P. 980,

41193 – DODOMA.

JUMATANO, APRILI 8, 2020.

7 thoughts on “Majaliwa Apokea Misaada kwa Ajili ya Mapambano Dhidi ya CORONA

 • August 11, 2020 at 7:51 am
  Permalink

  I loved as much as you’ll receive carried out right here.

  The sketch is tasteful, your authored material
  stylish. nonetheless, you command get got an edginess over that you wish be delivering the following.
  unwell unquestionably come more formerly again as exactly the same nearly a
  lot often inside case you shield this hike.

  Reply
 • August 14, 2020 at 5:30 pm
  Permalink

  I wanted to thank you for this excellent read!!
  I certainly enjoyed every little bit of it. I have you book marked
  to look at new stuff you post…

  Reply
 • August 31, 2020 at 1:06 am
  Permalink

  Hello I am so thrilled I found your webpage, I really found you by error, while I was searching on Askjeeve for something else, Regardless I am here now and would just like to say
  cheers for a fantastic post and a all round entertaining blog (I also love
  the theme/design), I don’t have time to browse it all at the moment but I have book-marked it and also added in your RSS feeds,
  so when I have time I will be back to read a lot more, Please do keep up the superb jo.

  Reply
 • September 5, 2020 at 10:59 am
  Permalink

  hello!,I like your writing so a lot! percentage we communicate extra approximately your article on AOL?
  I require an expert in this space to resolve my problem. May be that is
  you! Having a look forward to peer you.

  Reply
 • January 17, 2021 at 9:35 pm
  Permalink

  Hello, i think that i saw you visited my website so i came to “return the favor”.I am trying to find things to enhance my web site!I suppose its ok to use a few of your ideas!!|

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama