Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Akabidhiwa Madarasa Yaliyojengwa na Serikali ya Japan

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na akikata utepe ikiwa ni ishara ya kupokea madarasa mapya yaliyojengwa kwa Msaada wa serikali ya Japan katika Shule ya Msingi ya Nyakato wilayani Bukoba, Oktoba 8, 2018. Kulia kwake ni Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini, Katsutoshi Takeda. Majengo ya shule hiyo yaliharibiwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa Kagera.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea funguo kutoka kwa Mwakilishi wa Balozi wa Japan Nchini, Katsutoshi Takeda ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa madarasa yaliyojengwa na serikali ya Japan katika Shule ya Msingi ya Nyakato wilayani Bukoba, Oktoba 9, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini, Bw. Katsutoshi Takeda wakiwa kwenye moja ya madarasa yaliyojengwa kwa ufadhili wa serikali ya Japan katika shule ya msingi ya Nyakato wilayani Bukoba ambayo iliharibiwa na tetemeko la ardhi. Madarasa hayo yalikabidhiwa kwa Waziri Mkuu, Oktoba 9, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kupokea madarasa yaliyojengwa kwa masada wa serikali ya Japan katika shule ya msingi ya Nyakato wilayani Bukoba ambayo iliharibiwa na tetemeko la ardhi la Kagera. Madarasa hayo yalikabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini, Bw. Katsutoshi Takeda, Oktoba 9, 2018.

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail