Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mafunzo ya PS3 Yaendeleo Mkoani Dodoma

Mwezeshaji kutoka Mradi wa Uimarishaji Sekta za Umma (PS3) Christopher Masaaka ambaye pia ni Afisa Uchumi kutoka Halmashauri ya Wangingómbe Mkoa wa Njombe akitoa mafunzo kwa moja ya kundi la washiriki wa mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Wagisha Ronald na Hussein Kiranga (Katikati) kutoka Taasisi ya GIZ-TGPSH.

Baadhi ya Maafisa Uchumi, Mipango na Makatibu Afya kutoka Manispaa ya Singida wakijadili jambo wakati wa mafunzo ya Mfumo wa kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa leo Mjini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi mbalimbali wakiwemo Maafisa Uchumi, Mipango na Makatibu Afya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Manyara wakifuatilia mafunzo ya Mfumo wa kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa yanayoratibiwa na Mradi wa Uimarishaji Sekta za Umma (PS3) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) leo Mjini Dodoma. (Picha na Beatrice Lyimo)

59 thoughts on “Mafunzo ya PS3 Yaendeleo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama