Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

MAELEZO Yakusanya Zaidi ya Milioni 354

Idara ya Habari – MAELEZO imekusanya jumla ya shilingi 354,190,750 sawa na asilimia 199 katika mwaka wa fedha 2021/2022.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hayo leo Mei 20, 2022,  bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2022/23 ya wizara hiyo.

“Idara ya Habari – MAELEZO ilikadiriwa kukusanya kiasi cha shilingi 178,017,222 kutokana na mauzo ya picha za viongozi Wakuu wa Nchi na picha ya Baba wa Taifa,  vitambulisho, machapisho na ada ya mwaka ya magazeti. Hadi kufikia Aprili 30, 2022, Idara imekusanya jumla ya shilingi 354,190,750 ambayo ni sawa na asilimia 199,” alifafanunua Nnauye.

7 thoughts on “MAELEZO Yakusanya Zaidi ya Milioni 354

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama