Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Madalali wa Minada Kusajiliwa Kielektroniki

Na. Rahma Taratibu na Hilda Mlay, SJMC, Mbeya.

Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa mfumo wa kielektroniki wa utoaji Leseni za Udalali na Uendeshaji minada ya hadhara ambao utawezesha uombaji na upatikanaji wa Leseni kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia simu za mkononi ili kuwaondolea wananchi adha na gharama ya kufuata leseni hizo Makao Makuu – Dodoma.

Akizungumza wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya, Msimamizi wa mali za Serikali wizarani hapo, Bw. George Killo, alisema kuwa mfumo huo utamuwezesha mwananchi kufanya usajili popote alipo hivyo kupata leseni yake kwa wakati.

“Mwombaji wa leseni ya udalali anapaswa kujisajili kupitia tovuti ya Wizara (www.mof.go.tz) na kisha kubonyeza kipengele cha GAMIS na kujisajili, kujaza taarifa zinazohitajika, kujaza fomu za maombi kikamilifu na kuwasilisha kwa Katibu Tawala wa Wilaya husika kwa ajili ya uhakiki na saini.” Alieleza Bw. Killo.

103 thoughts on “Madalali wa Minada Kusajiliwa Kielektroniki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama