Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Madaktari na Wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Wajifunza Jinsi ya Kuokoa Maisha ya Mtu Aliyepata Tatizo la Dharula la Kiafya

Madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakijifunza jinsi ya kuokoa maisha ya mtoto aliyepata tatizo la dharula la kiafya wakati wa mafunzo ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano Taasisi hiyo jijii Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanatolewa na wataalamu kutoka kituo cha Emergency Medical Services Academy kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Sylivester Fanya kutoka kituo cha Emergency Medical Services Academy kilichopo Mkocheni jijini Dar es Salaam akiwafundisha madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kuokoa maisha ya mtu aliyepata tatizo la dharula la kiafya wakati wa mafunzo ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea umuhimu wa mafunzo ya jinsi ya kuokoa maisha ya mtu aliyepata tatizo la dharula la kiafya kwa washiriki wa mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoandaliwa na kituo cha Emergency Medical Services Academy kilichopo mikocheni jijini Dar es Salaam.
Picha na JKCI

229 thoughts on “Madaktari na Wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Wajifunza Jinsi ya Kuokoa Maisha ya Mtu Aliyepata Tatizo la Dharula la Kiafya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama