Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

JKCI na BMH Waanza Uchunguzi wa Mishipa ya Damu ya Moyo kwa Mtambo wa Cathlab

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma pamoja na timu ya wataalamu wa Taasisi hiyo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization) kupitia tundu dogo linalitobolewa kwenye paja. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Dkt. Alphonce Chandika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwafundisha wataalamu wa afya wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma kuhusu madhara ya moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure) kabla ya kuanza kwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa wagonjwa kupitia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.

Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakimfanyia mgonjwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.

Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumaliza kufanya uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa mgonjwa wa kwanza kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail