Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Maafisa Ustawi Waomba Ushirikiano Vita ya Ukatili

Na WMJJWM, DSM

Maafisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam wameiomba Jamii kutoa ushirikiano katika kufuatilia na kushughulikia kesi za vitendo vya ukatili ili lengo la kutokomeza vitendo hivyo lifikiwe.

Hayo yamebainika wakati wa kikao kazi kati ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima na Maafisa hao kilichofanyika jijini Dar es Salaam chenye lengo la kutathmini utendaji kwenye kutokomeza vitendo vya ukatili alipofanya ziara mkoani hapo tarehe 05 Oktoba, 2022.

Mmoja wa Afisa Ustawi wa Jamii, Suzan Boniphace amesema wanakutana na changamoto nyingi zinazokwamisha utendaji wao ikiwemo kukosa ushirikiano wa wanajamii na wadau wengine.

“Mara nyingi tunapoanza kufuatilia kesi tunajikuta zinaishia njiani kwa kukosa ushirikiano, wengine kesi zinaishia nyumbani na wakati mwingine wenzetu wa Mamlaka nyingine kutukwamisha”, alisema Suzana

9 thoughts on “Maafisa Ustawi Waomba Ushirikiano Vita ya Ukatili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama