Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Maafisa Ugani Watakiwa Kuwa Karibu na Wafugaji

Na Mbaraka Kambona, Arusha

Wafugaji wanaofanya shughuli zao Kanda ya Kaskazini wameiomba Serikali kuhakikisha Maafisa Ugani wanawafikia Wafugaji kwa urahisi ili kuwapatia huduma stahiki wakati wote ili ufugaji wao uwe bora na wenye tija.

Wakiongea kwa nyakati tofauti katika Maonesho ya Wakulima NaneNane Kanda ya Kaskazini yanayofanyika mkoani Arusha Agosti 4, 2022, Wafugaji hao walisema ni muhimu Maafisa Ugani kuwatembelea wafugaji kila wakati na kutatua changamoto zinazowakabili kwani kufanya hivyo kutasaidia kuboresha ufugaji wao na manufaa ya kazi hiyo yataonekana.

Mfugaji kutoka Arusha, Bw. Desderi Kimario alisema kuwa wanahitaji Maafisa Ugani wa kilimo na mifugo wote kwa pamoja wawe wanafanya kazi karibu na wafugaji ili wafugaji hao waweze kufanya shughuli zao kwa kuzingatia ushauri wa Wataalamu hao na kufanya ufugaji wao uwe na tija kubwa kwao  na nchi kwa ujumla.

30 thoughts on “Maafisa Ugani Watakiwa Kuwa Karibu na Wafugaji

Leave a Reply to Hellyjar Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama