Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Maafisa Ugani Watakiwa Kuwa Karibu na Wafugaji

“Tunaomba Maafisa Ugani wawe wanatutembelea mara kwa mara sisi wafugaji wadogowadogo katika maeneo yetu huku kwenye Kata na Vijijini ili kujua matatizo yetu na sio mpaka tufike kwenye maonesho kama hivi, kwa sababu maonesho huwa ni mara moja kwa kila mwaka”, alisema Kimario

Bw. Lawrence Kimambi, Mfugaji kutoka Mkoa wa Kilimanjaro alisema  kwa sasa ardhi imekuwa finyu hivyo ni muhimu wafugaji wakaendelea kupatiwa elimu ya kulima malisho ya mifugo ili kuokoa changamoto ya malisho na kuleta manufaa zaidi kwa jamii za wafugaji na nchi kwa ujumla.

Naye Kevin Manase kutoka Arusha alisema kuwa kama wafugaji wataendelea kuelimishwa vizuri kuhusu umuhimu wa ulimaji wa malisho ya mifugo basi sio muda mrefu migogoro kati ya wakulima na wafugaji itakwisha.

Kwa Upande wake, Afisa Mifugo Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo, Bw. Israel Kilonzo aliwashauri wafugaji hao kuanza kujifunza namna ya  kustawisha malisho ya mifugo na kuachana na tabia ya kutegemea malisho ya asili peke yake  kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza migogoro ya ardhi.

“Kama tunavyojua watu wanaongezeka na mifugo pia inaongezeka na ardhi iliyopo haitoshi kufanya ufugaji wa kuhamahama, ni lazima tujifunze kustawisha malisho  katika maeneo yetu na tujifunze kuyatumia vizuri ikiwemo kuwa na mifugo tutakayoimudu kuihudumia”, alisema Kilonzo.

30 thoughts on “Maafisa Ugani Watakiwa Kuwa Karibu na Wafugaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama