Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Maafisa Habari wa Serikali Watoa Msaada wa Milioni 7.5 Kusaidia Wazee Bukumbi

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Maafisa Habari wa Serikali wametoa msaada wenye thamani ya jumla ya shilingi 7, 507,700 katika Makao ya Wazee Wasiojiweza yaliyopo Bukumbi jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) Paschal Shelutete (mwenye tshirt nyeupe) akikabidhi moja ya magodoro yaliyotolewa na Chama cha Maafisa Serikali kwa kituo cha wazee Bukumbi Jijini Mwanza.

Msaada huo  imetolewa leo ikiwa imejumuisha vitu mbalimbali vikiwemo vyandarua 88, magodoro 88, mashuka 176, mabeseni 88, mchele kilo 110 na mafuta ya kupikia lita 40 vilivyogharimu jumla ya shilingi 6,085,700 huku fedha taslim shilingi 1,422,000 zikichangwa papo kwa papo.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Habasi akizungumzia jinsi Maafisa Mawasiliano walivyoguswa na Kuamua kuwasaidia Wazee wa kituo cha makao ya wazee na wasio jiweza kilichopo Bukumbi Wilayani Misungwi walipowatembelea leo katika eneo la Bukumbi Wilayani Misungwi.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa serikali ya Awamu ya Tano inafanya juhudi mbalimbali za kuwasaidia wazee nchini.

“Kwa kuwa serikali inaendelea kuboresha maisha ya wazee wasiojiweza walioko katika makazi yao, na kwa kuwa Maafisa Habari wa Serikali ni moja ya wanaounga mkono juhudi hizo, kwa pamoja tumeamua kuja kwa ajili ya kuwasaidia wazee hawa”, alisema Dkt. Abbas.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari wa Serikali (TAGCO), Bw. Pascal Shelutete amesema kuwa jukumu la kulinda wazee ni la jamii nzima hivyo anawashukuru Maafisa Habari wa Serikali kwa kuamua kwenda kuwatembelea wazee hao.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Habasi akikabidhi chandarua kwa mmoja wa wazee wa kituo cha makao ya wazee na wasiojiweza kilichopo Bukumbi Jijini Mwanza.Kulia kwake ni Afisa Ustawi wa Jamii Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto Bi.Ferejiana Kiromo.Kwa upande wake Afisa Mfawidhi Makao ya Wazee Wasiojiweza, Leah Mwakajobe amefafanua kuwa makazi hayo yana jumla ya watu 88 ambapo kati ya hao wazee ni 73 na watoto ni 15.

Afisa Mfawidhi wa Makao ya Wazee na Wasiojiweza Bukumbi Bi.Leah Mwakatobe akitoa neno la shukrani kwa Uongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) baada ya kuwatembelea na kuwapa msaada wa Magodoro, Mashuka, Vyandarua, Mabeseni, Vyandarua ,Mchele na Mafuta.

Baadhi ya Wazee walio katika makao ya wazee na wasio jiweza kilichopo Bukumbi wakiwa pamoja na Maafisa habari wa Serikalini mara baada ya kuwatembelea katika kituo chao leo katika eneo la Bukumbi Jijini Mwanza.

“Kwa kuwa serikali inawajali wazee na kuendelea kuwapa misaada mbalimbali, natoa rai kwa wananchi kuwapenda na kuwajali wazee hao kwani baadhi yao waliitumikia nchi hii kwa nguvu zao zote,”alisema Bi. Leah.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bi.Sarah Kibonde akimkabidhi beseni mmoja ya wazee wa kituo cha wazee Bukumbi leo Jijini Mwanza.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abasi akimkabidhi Afisa Mfawidhi wa Makao ya Wazee na Wasiojiweza Bukumbi Bi.Leah Mwakatobe kiasi cha shilingi milioni moja laki nne na elfu ishirini na mbili ilkiwa ni michango ya Maafisa habari Serikalini walipotembelea kituo cha wazee Bukumbi Jijini Mwanza.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail