Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Jijini Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akihutubia hadhira ya wafanyakazi wa Serikali, Taasisi za Umma na Sekta binafsi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Tanzania ya Uchumi wa Kati Inawezekana, Wakati wa Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi ni Sasa.”

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (katikati) pamoja na viongozi wengine wakishiriki kuimba wimbo maalum wa umoja na mshikamano wa wafanyakazi alipokuwa mgeni rasmi maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mkoa wa Dodoma leo katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Tanzania ya Uchumi wa Kati Inawezekana, Wakati wa Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi ni Sasa.” Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula.

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), wakiimba wimbo maalum wa umoja na mshikamano wa wafanyakazi wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Kimkoa leo katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Tanzania ya Uchumi wa Kati Inawezekana, Wakati wa Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi ni Sasa.”

Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa maandamano ya wafanyakazi katika kusherehekea Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani mkoani Dodoma leo. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Tanzania ya Uchumi wa Kati Inawezekana, Wakati wa Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi ni Sasa.”

Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wakiwa katika maandamano ya wafanyakazi katika kusherehekea Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani mkoani Dodoma leo. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Tanzania ya Uchumi wa Kati Inawezekana, Wakati wa Mishahara