Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Kilimo Mseto ni Ukombozi wa Uhakika wa Chakula Nchini-Kusaya


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya ( katikati) akikagua akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Dkt. Vicent Naano (kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bi. Karoline Mthapula (kulia) leo alipowasili kwenye viwanja vya maonesho ya Kilimo Mseto mjini Musoma ambapo ameyafungua rasmi.

Na Mwandishi wetu- Wizara ya Kilimo

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya leo ( 19.11.2020) amewasili mkoani Mara na kuzindua maonesho ya siku tatu ya kuhamasisha wakulima na wafugaji nchini kutumia kilimo mseto ili kuongeza uhakika wa chakula na kipato.
 
Maonesho ya Kilimo Mseto yanafanyika mjini Musoma kwa kuwashirikisha wakulima, wafugaji na wavuvi chini ya uratibu wa shirika la Vi Agroforestry pamoja na taasisi za serikali na wadau wa sekta ya kilimo.
 
” Nimekuja hapa Mara kuwatia moyo wakulima waendelee kujikita katika kilimo mseto kwa kuwa kinafanya vema katika kuhakikisha kaya na taifa linajitosheleza kwa chakula” alisema Kusaya.
 
Kusaya aliongeza kusema wizara ya kilimo inaendelea kujanga mazingira wezeshi kwa wakulima kupata elimu na teknolojia bora ili kilimo kiwe na tija na kukuza uchumi  hivyo uwepo wa maonesho haya una mchango mkubwa kwa wakulima.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *