Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Chatembelea Eneo Lililotengwa kwa Ajili ya Mji wa Serikali

Katibu wa Kikosi kazi cha kitaifa cha Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akieleza jambo kwa wajumbe wa kikosi kazi hicho hiyo walipotembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya  Mji wa Serikali.

Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania wakiweka nguzo ya umeme katika eneo la Ihumwa ambalo limetengwa kwa ajili ya mji wa serikali Dodoma.

Mjumbe wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Nigel Msangi akipata maelezo ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Mji wa Serikali kwa Kikosi kazi kutokana na ramani ya Mji wa Serikali walipotembelea kukagua eneo hilo Ihumwa, Dodoma.

Afisa Mipango Miji Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bw.William Alfayo akiwaonesha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Mji wa Serikali kwa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma walipotembelea eneo hilo Juni 7, 2018

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma wakiangalia maeneo mbalimbali yaliyotengwa kulingana na ramani ya Mji mpya wa Serikali Ihuma Dodoma.

 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail