Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

KICHERE: NITAFANYA KAZI KULINDA MATUMIZI YA KODI ZA WATANZANIA

AG aliyemaliza Muda wake Prof. Mussa Assad akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari(Hawapo pichani) kuhusu makabidhiano ya Ofisi ya Mkaaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG), yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, kushoto ni CAG mpya, Bw. Charles Kichere

Na.Mwandishi Wetu

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Bw. Charles Kichere amesema kuwa ataendelea kutekeleza majukumu ambayo yameachwa na CAG aliyemaliza muda wake Prof.Mussa Assad kwani Ofisi hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya watanzania.

Akizungumza katika makabidhiano Kichere alisema kuwa Ofisi ya CAG ni nguzo muhimu kwa watanzani kwani ndiyo ofisi inayolinda na kuangalia matumizi sahihi ya kodi yao wanayolipa kila siku.

CAG aliyemaliza Muda bedava bonus adana escort mersin escort canlı bahis oyna bedava bonus veren bahis siteleri hoşgeldin bonusu wake Prof. Mussa Assad Akimkaribisha CAG mpya, Bw. Charles Kichere Kabla ya Makabidhiano ya Ofisi ya Mkaaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG), yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam

“Tutaendelea kuifanyakazi ambayo imefanywa na Prof.Assad na timu yake, nitahakikisha kushirikiana na wafanyakazi wa Ofisi hii kuifanya kazi hii ya kulinda mapato ya kodi ya watanzania”, Alisema Kichere.

Kichere alisema kuwa katika kutekeleza majukumu hayo mapya atahakikisha kuwa atalinda Kodi ya watanzania wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wafanyakazi ili fedha inayopataikana kwenye kodi iweze kuwanufaisha wote.

CAG aliyemaliza Muda wake Prof. Mussa Assad akimueleza jambo CAG mpya Bw. Charles Kichere katika Makabidhiano ya Ofisi ya Mkaaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG), yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Aliwahakikishia watanzania kuwa hakuna kodi inayotolewa na watanzania ambayo itapotea kwa hiyo ataangalia na kuilinda  kwaajili ya kuwaletea maendeleo.

“Nataka kufanya kazi kulinda maslahi ya watanzania nimefanyakazi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA najua ugumu wa kukusanya kodi na kupata mapato, kwa hiyo nitahakikisha kuwa nailinda kodi ya wananchi kwa wivu mkubwa sana”, Alisisitiza Kichere.

CAG aliyemaliza Muda wake Prof. Mussa Assad akimkabidhi nyaraka za Ofisi CAG mpyaBw. Charles Kichele katika Makabidhiano ya Ofisi ya Mkaaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG), yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake CAG aliyemaliza muda wake Prof. Mussa Assad alisema kuwa ataendelea kushirikiana na Ofisi hiyo licha ya kustaafu lakini atakuwepo kwa wakati ambao atahitajika kutoa msaada kutokana na uzoefu na ujuzi aliopata kwa muda wa miaka mitano akiwa anatumikia Ofisi hiyo.

“Nataka nikuambie CAG mpya ukihitaji msaada wa kitu chochote kiwe cha binafsi au cha kiofisi, ujuzi na uzoefu wa kazi hii niko tayari kushirikiana na wewe na utapata msaada huo kwa haraka”, Alisema Prof. Assad.

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail