Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Kazi Inaendelea, Dkt. Abbasi Akabidhi Gari Idara ya Habari – MAELEZO Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi ufunguo wa gari Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Rodney Thadeus wakati wa makabidhiano ya gari hilo  jijini Dodoma. Idara ya Habari –MAELEZO imekabidhiwa gari hilo aina ya Noah ili kuongeza ufanisi wa shughuli za idara hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akikagua gari wakati wa kukabidhi gari hilo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Rodney Thadeus  jijini Dodoma. Gari hilo aina ya Noah limekabidhi kwa Idara ya Habari – MAELEZO ili kuongeza ufanisi wa Idara hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Rodney Thadeus (kulia) na Afisa Tawala wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mussa Varisanga wakiangalia namna Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akiendesha gari wakati wa kukabidhi gari hilo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Rodney Thadeus  jijini Dodoma. Idara ya Habari –MAELEZO imekabidhiwa gari hilo aina ya Noah ili kuongeza ufanisi wa shughuli za idara hiyo.

Afisa Tawala wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mussa Varisanga (katikati) akielezea jambo wakati wa makabidhiano ya gari baina ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi(kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Rodney Thadeus (kulia) leo jijini Dodoma. Idara ya Habari –MAELEZO imekabidhiwa gari hilo aina ya Noah ili kuongeza ufani wa shughuli za idara hiyo.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail