Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Katibu Mkuu Uchukuzi Awataka TAA Kujipanga

Katibu Mkuu Migire amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya viwanja vya ndege nchini ili kuwawezesha wasafirishaji kuamua njia wanayotaka kusafirisha mizigo, bidhaa na abiria na hatimaye kuchochea maendeleo. 

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Uwanja huo, Matha Chidodo  amesema tabia nchi imekuwa ikiathiri miundombinu ya kiwanja hicho hususani uzio ambao umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la maji katika Ziwa Viktoria. 

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Migire amekagua miundombinu ya bandari ya Bukoba na kuutaka uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha miundombinu hiyo inaboreshwa sambamba na ujio wa kukamilika kwa ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza. 

Naye Kaimu Meneja Bandari ya Bukoba amesema mradi wa upanuzi wa miundombinu uko katika bandari za Bukoba, Kemondo na Mwanza uko katika hatua za mwisho za manunuzi na kumuhakikishia Katibu Mkuu kuwa kabla ya meli mpya kuanza kutoa huduma mradi utakuwa umekamilika. 

Katibu Mkuu Migire yupo mkoani Kagera kukagua miundombinu na miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya Sekta hiyo.

2 thoughts on “Katibu Mkuu Uchukuzi Awataka TAA Kujipanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama