Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Katibu Mkuu Uchukuzi Awataka TAA Kujipanga

Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migire amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha anaweka mpango mkakati wa ujenzi wa uzio imara wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba ili kuongeza usalama kiwanjani hapo. 

Ametoa kauli hiyo mjini Kagera mara baada ya kutembelea kiwanja hicho na kubaini changamoto ya uzio iliyotokana na changamoto za tabianchi  na kuwataka kuzingatia kanuni na taratibu zinazoongoza usafiri wa anga. 

“Ni jukumu lako kama Meneja kuwasilisha changamoto hii Makao Makuu ili waje na mipango endelevu kwa changamoto hii sababu kwenye wizara hii tuna taasisi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), zungumzeni nao ili kupata taarifa za nyuma ili kuweka mipango ambayo itanusuru miundombinu  hii”, amesema Katibu Mkuu Migire. 

2 thoughts on “Katibu Mkuu Uchukuzi Awataka TAA Kujipanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama