Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Ashiriki Warsha Kuhusu Mifumo ya Tehama

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Miundombinu ya TEHAMA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Baltazari Kibola wakati wa warshaa kuhusu Mifumo ya TEHAMA na Takwimu inavyotegemeana Kiutendaji yaliyofanyika Tarehe 04 Januari, 2018 Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akiweka sahihi katika kitabu cha wageni katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) aliposhiriki Warsha ya Masuala ya Mifumo ya (TEHAMA) yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo Januari 4, 2018 Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Mohamed Pawaga akizungumza jambo alipotembelewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora katika ofisi yake Mjini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Miundombinu ya TEHAMA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Baltazari Kibola akiwasilisha mada kwenye warsha ya masuala ya Mifumo ya TEHAMA yaliyoandaliwa na ofisi hiyo Januari 04, 2018

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akitoa ufafanuzi wa masuala ya mifumo ya TEHAMA wakati wa Warsha iliyolenga juu ya Mifumo ya TEHAMA na Takwimu inavyotegemeana Kiutendaji yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TAMISEMI Dodoma .

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Mohamed Pawaga akieleza umuhimu wa matumizi ya Mifumo ya TEHAMA na Takwimu kwa wajumbe wa warsha iliyoandaliwa na Ofisi hiyo Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa Warsha wakifuatilia uwasilishaji kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Miundombinu ya TEHAMA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Baltazari Kibola wakati wa mafunzo ya masuala ya TEHAMA yaliyofanyika katika Ofisi za TAMISEMI Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya masuala ya Mifumo ya TEHAMA kwa Kaimu Mkurugenzi wa masuala ya Miundombinu ya TEHAMA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Baltazari Kibola wakati wa warsha ya masuala ya Mifumo ya TEHAMA iliyofanyika Dodoma. (Picha Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu – Dodoma)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *