Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Katibu Mkuu Mambo ya Ndani Meja Jenerali Kingu Akagua Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (Wa pili kushoto), akikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dodoma leo.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akipokea maelezo kutoka kwa Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza jinsi ujenzi unavyoendelea wakati ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dodoma leo.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akitoa maelekezo kwa Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji baada ya kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dodoma leo. (Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

338 thoughts on “Katibu Mkuu Mambo ya Ndani Meja Jenerali Kingu Akagua Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama