Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Katibu Mkuu Bibi Susan Mlawi Awapongeza Washiriki wa Multichoice Talent Factory Academy kwa Kuiwakilisha Vyema Nchi.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawi akizungumza na Vijana wanne (hawapo katika picha ) waliorejea kutoka nchini Kenya walikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmoja yaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawati lijulikanalo kama “Multichioce Talent Factory Academy”walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara hiyo Bw.Mussa Nyoni na kushoto ni Bibi Jane Moshi ambaye ni Muongozaji wa Filamu (Producer) kutoka katika Academy hiyo.

Na Shamimu Nyaki – WHUSM

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi amewapongeza vijana wanne waliofanya vizuri katika mafunzo ya uaandaaji wa Filamu yalioandaliwa na Kampuni ya Multichoice yaliyofanyika nchini Kenya ambapo amewataka kutumia taaluma waliyopata kutengeneza filamu bora zenye maudhui ya kuitangaza nchi yetu na kuleta ushindani katika soko.

Katibu Mkuu Bibi. Susan ameyasema hayo leo ofisini kwake Jijini Dodoma baada ya kutembelewa na vijana hao ambao amewataka kufika katika Bodi ya Filamu Tanzania kuwasilisha uelewa waliopata na kushauri namna ambavyo Bodi hiyo inaweza kuwatumia katika tasnia hiyo.

Meneja Biashara kutoka Kampuni ya Multichoice Bw.Jonson Mshana (kulia) akitoa maelezo mafupi kuhusu “Multichioce Talent Factory Academy” iliyodhamini vijana wanne katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmoja yaliyoandaliwa na Kampuni hiyo Nchini Kenya walipofika ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi (kulia) kuelezea namna walivyonufaika na mafunzo hayo.

Bw. Jamal Mohamed Kishuli ambaye ni miongoni mwa Vijana wanne waliorejea kutoka nchini Kenya walikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmoja yaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawati lijulikanalo kama “Multichioce Talent Factory Academy” akizumngumza wakati walipomtembelea Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawi ofisini kwake Jijini Dodoma.

“Nawapongeza sana kwa kufanya vizuri katika mafunzo mliopewa,naamini mtayatumia vizuri katika kukuza vipaji vyenu na kusaidia mawazo kwa wengine ambao hawajapata nafasi hii,Lakini pia mtatumia ujuzi na taaluma mliyopata katika kuleta mapinduzi ya utengenezaji wa filamu hapa nchini”alisema Bibi Susan.

Naye Meneja wa masuala ya Biashara wa Kampuni ya Multichoice Bw.Jonson Mshana amesema kuwa Kampuni hiyo imeanzisha dawati la kusaka vipaji vya uandaaji wa kazi za filamu (Multichoice talent Factory Academy) kwa Bara la Afrika ili vijana wenye uwezo na vipaji kupata fursa ya kuongezewa maarifa pamoja na kutafuta ajira kwa njia rahisi.

Bw.Wilson Nkya miongoni mwa Vijana wanne waliorejea kutoka nchini Kenya walikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmoja yaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawati lijulikanalo kama “Multichioce Talent Factory Academy” akizumngumza wakati walipomtembelea Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawi (hayupo katika picha) ofisini kwake Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na Vijana waliorejea kutoka nchini Kenya walikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmoja yaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawati lijulikanalo kama “Multichioce Talent Factory Academy” baada ya kupokea taarifa ya mafunzo waliyopata walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma.

Bw.Jonson ameongeza kuwa Kampuni hiyo kila mwaka inatafuta vijana wanne ambao wanapatikana kwa kuomba nafasi hiyo na hatimaye kufanyiwa usaili na kujiunga na wenzao kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Kenya,Ethiopia, Uganda na Nigeria.

Naye Kijana Jamal Mohamed Kishuli ambaye amejifunza “Art Designer” amesema kuwa vijana wanapaswa kujiamini katika kila wanachokifanya na kutokata tamaa lakini pia zinapotokea fursa za kuonyesha uwezo wao basi wasisite kujitokeza ili kupata nafasi ya kujitangaza kupitia vipaji walivyonayo.

Vijana hao walikua katika mafunzo ya Uandishi wa Mswada (Script Writer), Uandaaji (producer) Uongozaji (Directing) na Art Desgner ambayo wamejifunza kwa mwaka mmoja katika Chuo Kikuu cha Kenyata nchini Kenya.

30 thoughts on “Katibu Mkuu Bibi Susan Mlawi Awapongeza Washiriki wa Multichoice Talent Factory Academy kwa Kuiwakilisha Vyema Nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama