Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza na uongozi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), (hawapo pichani), wakati wa ziara yake kwa wakala huo, mkoani Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amewataka wahandisi, wakandarasi, wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi kuongeza ubunifu na kuzingatia maadili katika majukumu yao ya kazi ili kuliwezesha Taifa kunufaika na thamani ya fedha katika miradi ya ujenzi inayoendelea.
Akizungumza mkoani Dar es Salaam, mara baada ya kutembelea taasisi za Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), amewataka wataalamu hao kufahamu kuwa maendeleo na ukuaji wa uchumi unategemea sana taaluma zao.
Pages: 1 2
As the admin of this web page is working, no hesitation very shortly it will be famous, due to its feature contents.|