Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Kamishna Ustawi wa Jamii Atembelea Kituo cha Wazee Kibirizi.

Afisa Mfawidhi wa kituo cha kulea Wazee cha Kibirizi Bw. Heradius Mushi (kulia) akifafanua mambo mbalimbali yanayohusu kituo hicho kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi (katikati) wakati Kamishna huyo alipokitembelea kituo hicho mapema wiki hii Mkoani Kigoma.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Rabikira Mushi (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa wazee waishio katika Kituo cha Kulea Wazee cha Kibirizi mkoani Kigoma, Bw. Said Lekegwa (kulia) na Bi.  Veronika Ramadhani (kushoto) mara baada ya kuwakabidhi zawadi ya sabuni.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail