Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Kamati za Michezo za Mikoa na Wilaya zaagizwa kuongeza kasi katika kukuza Michezo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati akifungua kikao cha tatu kati ya Michezo la Michezo la Taifa na Kamati za Maendeleo ya Michezo za Mikoa kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 21 -22 jijini Dodoma.

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameziagiza Kamati za Michezo za Mikoa na Wilaya kuongeza kasi katika kukuza na kuendeleza michezo nchini.

Dkt. Mwakyembe ametoa agizo hilo leo Jijini Dodoma wakati alipofungua kikao cha tatu kati ya Baraza la Michezo la Taifa na Kamati za Maendeleo ya Michezo za Mikoa kinachofanyika kwa siku mbili jijini hapo.

“Sekta ya michezo inasaidia kuimarisha Afya, kujenga urafiki na umoja lakini pia ni ajira ambayo haina ushindani wa kipato hivyo ni wajibu wenu kama viongozi wa sekta hii kutafuta namna bora ya kusaidia uboreshaji wa sekta hii”.alisema Dkt. Mwakyembe.

 

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Alex Nkenyenge akionesha  Sera ya Michezo ya Taifa ya mwaka 1995 katika kikao cha tatu kati ya Baraza la Michezo la Taifa na Kamati za Maendeleo ya Michezo za Mikoa kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 21-22 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa kikao cha tatu kati ya Baraza la Michezo la Taifa na Kamati za Maendeleo ya Michezo za Mikoa kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 21- 22 jijini Dodoma wakifuatilia kikao hicho.

Mhe. Waziri ameongeza kuwa Taifa kwa sasa limeanza kupata mafanikio katika michezo kwa kuwa na wanamichezo wengi wanaojituma ambao wamepata nafasi ya kucheza soka nje ya nchi lakini pia kumekua na ongezeko la wawakilishi wengi katika mashindano ya kimataifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Leordigar Tenga amesema kuwa Kikao Kazi hicho kina lengo la kufanya tathmini kutengeneza mpango mkakati wa   maendeleo ya michezo nchini.

Aidha Mwenyekiti huyo ameshauri Serikali kuongeza bajeti ya michezo pamoja na kuajiri wataalamu zaidi wa sekta hiyo.

Naye Afisa Michezo wa Mkoa wa Lindi Bw. Chiza Joseph ameshauri kuwepo na Idara ya Michezo inayojitegemea ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa,Mkatibu Tawala wa Mikoa pamoja na Maafisa Michezo wa Mikoa baada ya kufungua kikao cha tatu kati ya Baraza la Michezo la Taifa na Kamati za Maendeleo ya Michezo za Mikoa kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 21-22 jijini Dodoma..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama