Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Kamati ya Miundombinu Yapongeza Sekta ya Ujenzi Utekelezaji wa Bajeti

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Selemani Kakoso, akizungumza na Viongozi pamoja na Watendaji wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Wakala huo, mjini Dodoma.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeipongeza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Sekta ya Ujenzi kwa kupeleka fedha za kutosha kulingana na bajeti iliyoidhinishwa kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ili kuuwezesha Wakala huo kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Selemani Kakoso, mjini Dodoma mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wakala huo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza Wakala kujipanga na kutekeleza kwa vitendo mipango waliyoianzisha badala ya kuishia kwenye makaratasi.

“Kamati imepaza sauti na fedha za kutosha mmeshapewa sasa mfanye kazi kwani  hatuhitaji mipango mizuri ya makaratasi bali tunataka vitendo”, amesisitiza Mwenyekiti huyo.

Aidha, ameitaka Wizara ishirikiane na Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha inasimamia madai ya kiasi cha zaidi ya Shilingi Bilioni 31 ambayo Wakala huo unadai Taasisi za Serikali na Wizara ili yalipwe kwa wakati.

Mwenyekiti ameongeza kuwa Wizara itizame katika mapana yake namna bora ya kupunguza gharama za ununuzi wa magari pamoja na vipuri vyake kwa kuwa lengo ni kuipunguzia gharama Serikali.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa mwaka wa fedha 2018/19, mjini Dodoma.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa Wakala huo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/19, Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amewaeleza wajumbe wa kamati hiyo kuwa TEMESA ilifanikiwa kukusanya mapato ya kiasi cha zaidi ya shilingi Bili 58 kutoka vyanzo vyake vya ndani vya mapato na ruzuku ya Serikali.

Ameongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha 2019/20 Wakala unatarajia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 89.

Naibu Waziri huyo amesema Wakala umeanzisha karakana katika ngazi ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ili kuhakikisha huduma inasogezwa karibu na wateja.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mjini Dodoma.

Ameongeza kuwa Wakala umenunua vitendea kazi vya kisasa ikiwemo gari lenye karakana (Mobile Workshop) ambalo litatoa huduma popote pale na pia Wakala ulikamalisha ukarabati wa karakana za Mkoa wa Singida, Dar es Salaam na Mwanza.

Naye Mbunge wa Misungwi, Mheshimiwa Charles Kitwanga, amesisitiza umuhimu wa usalama wa abiria na mizigo katika vivuko kwa kuweka  na mifumo madhubuti ya kuonesha idadi kamili ya abiria na uzito wa mizigo ili kuepusha ajali zinazoweza epukika.

Kikao cha Kamati hiyo kimeshirikisha wajumbe mbalimbali ikiwemo Naibu Waziri wa Sekta ya Ujenzi  Elias Kwandikwa, Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga ambapo taarifa ya utekelezaji ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ambayo inatokana na maazimio ya vikao vya Bunge vilivyopita imejadiliwa na kupokelewa.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Viongozi na Watendaji kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), wakiwa katika kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya Wakala huo na utekelezaji wa maazimio ya kamati hiyo, mjini Dodoma.

 

10 thoughts on “Kamati ya Miundombinu Yapongeza Sekta ya Ujenzi Utekelezaji wa Bajeti

 • August 11, 2020 at 3:29 pm
  Permalink

  Hi just wanted to give you a brief heads up and let you know a
  few of the pictures aren’t loading properly. I’m not sure why but I think its a linking issue.
  I’ve tried it in two different browsers and both show the same
  outcome.

  Reply
 • August 25, 2020 at 2:13 am
  Permalink

  Fine way of describing, and fastidious article to take facts concerning my presentation subject matter, which i am going to deliver in school.
  cheap flights 31muvXS

  Reply
 • August 27, 2020 at 6:16 am
  Permalink

  you are truly a good webmaster. The site loading velocity is amazing.
  It sort of feels that you’re doing any distinctive trick. Also, The
  contents are masterwork. you have done a excellent activity in this
  topic!

  Reply
 • August 27, 2020 at 7:39 am
  Permalink

  What’s up all, here every person is sharing such familiarity, so it’s good to read this webpage,
  and I used to visit this website all the time.

  Reply
 • August 28, 2020 at 7:51 am
  Permalink

  It’s going to be end of mine day, except before finish
  I am reading this wonderful post to improve my knowledge.

  Reply
 • August 28, 2020 at 8:19 am
  Permalink

  Hey there just wanted to give you a brief heads
  up and let you know a few of the pictures aren’t loading correctly.
  I’m not sure why but I think its a linking issue. I’ve
  tried it in two different web browsers and both show the same results.

  Reply
 • October 26, 2020 at 10:34 am
  Permalink

  Could you transfer $1000 from my current account to my deposit account? revistas pdf mega mexico In the absence of such a hearing, a dog owner’s only option in a case of dog-on-dog violence is to file a civil suit against the owners of the attacking mongrel — but such suits are usually unsuccessful.

  Reply
 • October 26, 2020 at 11:13 am
  Permalink

  I’d like to withdraw $100, please buy diclofenac sodium uk “So I would ask either one of you what are the special plans in the president’s action plan to help address these people who are losing their jobs, ” Rep. Ed Whitfield (R-Ky.) asked EPA Administrator Gina McCarthy and Energy Secretary Ernest Moniz.

  Reply
 • October 27, 2020 at 11:14 am
  Permalink

  Punk not dead tylenol or advil for lower back pain Just as high frequency trading, via automated software, took over the financial markets in the early 2000s, the use of bots is a technique that is increasingly coming to dominate online sales of all stripes.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama