Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

JMP Ashinda kwa Kishindo Uchaguzi Mkuu 2020.


Zoezi la Utangazaji wa Matokeo ya Jumla ya Uchagzui wa Rais 2020, likiendeleo katika Kituo cha Mikutano kimataifa Julisu Nyerere(JNICC), Jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage, amemtangaza Dkt.John Pombe Magufuli wa CCM kuwa mshindi wa kiti hicho kwa kura zaidi ya 12,516,252 sawa na asilimia 84.4.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji  Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akitangaza   matokeo ya jumla  Uchaguzi wa Rais ambapo Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt.John Pombe Magufuli ameshinda kwa zaidi ya kura  milioni 12, kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera

Wakala wa moja kati ya vyama 15 ambavyo vimeshiriki Uchaguzi wa Rais 2020 akisoma fomu ya matokeo kabla ya kuijaza katika  zoezi la utangazaji wa matokeo ya jumla kwa Uchaguzi wa Rais 2020 kukamilika.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji  Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akitangaza   matokeo ya jumla  Uchaguzi wa Rais ambapo Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt.John Pombe Magufuli ameshinda kwa zaidi ya kura  milioni 12.

Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera akikabidhi fomu ya matokeo kwa mmoja kati ya mawakala wa vyama vilivyoshiriki Uchaguzi wa Rais 2020, ili aisome na kusaini kukubali matokeo ya Uchaguzi huo.

1,998 thoughts on “JMP Ashinda kwa Kishindo Uchaguzi Mkuu 2020.