Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Jaji Mutungi: Zoezi la Uhakiki wa Vyama Halifuti Chama cha Siasa

1. Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Mhe .Jaji, Francis Mutungi akifafanua jambo wakati wa Mkutano wake na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa kuhusu zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (ORPP) inatarajia kufanya zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini kuanzia tarehe 17 Machi, 2020. Kushoto ni Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Mohamed Ally Ahmed.

Na Mwandishi Wetu

MSAJILI wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Mstaafu Francis Mutungi amesema zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa linalotarajia kuanza tarehe 17 Machi mwaka huu, halina malengo ya kufuta usajili wa vyama hivyo na badala yake ni utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019.

Jaji Mutungi aliyasema hayo leo Jumanne (Machi 10, 2020), wakati wa Mkutano wake na Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu nchini uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Bunge Jijini Dar es Salaam.

Jaji Mutungi alisema malengo ya zoezi hilo litakoendeshwa na Ofisi yake  ni kuona namna bora ya kujenga uelewa wa pamoaj wa sheria ya vyama hivyo katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

2. Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Mhe .Jaji, Francis Mutungi akifafanua jambo wakati wa Mkutano wake na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa kuhusu zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (ORPP) inatarajia kufanya zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini kuanzia tarehe 17 Machi, 2020.

Alisema kuwa ni wajibu wa vyama vyote vya siasa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo na kuwa Serikali haiwezi kuahirisha zoezi hilo na badala yake kuvitaka vyama hivyo iwapo vina hoja ya msingi ni vyema zikawasilisha katika Baraza la Vyama hivyo ili kuweza kupatiwa mwafaka wa pamoja wa makubaliano.

Kwa mujibu wa Jaji Mutungi alisema katika muda uliobaki kuelekea uchaguzi mkuu, kwa mujibu wa sheria Ofisi yake haiwezi kufuta usajili wa chama chochote cha siasa na hivyo kuwataka Viongozi wa vyama vya siasa kuondoa dhana potofu kuwa Serikali imepanga kufuta baadhi ya vyama vyenye usajili wa kudumu nchini kutoka katika daftari la Msajili wa Vyama vya siasa.

3. Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ally Ahmed akifafanua jambo mbele ya Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa nchini wakati wa Mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa (RPP), Mhe. Jaji, Francis Mutungi (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo. Mkutano huo ulihusu kuwapitisha viongozi hao katika hatua zitakazopitiwa wakati zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa. Linalotarajiwa kuanza tarehe 17, Machi 2020

Aliongeza kuwa zoezi la uhakiki linaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kuwa zoezi hilo si geni kwa kuwa serikali imekuwa ikiendesha zoezi la uhakiki wa taasisi, makampuni na mashirika mbalimbali na hivyo kwa vyama vya siasa zoezi hilo halina utofauti wowote kama ilivyo kwa taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Jaji Mutungi alisema hakuna sababu ya vyama hivyo kujenga hofu kuhusu zoezi hilo kwani limekusudia kubaini changamoto mbalimbali zinazovikabili vyama vya siasa nchini ili kuweza kutoa mapendekezo kwa Serikali na hivyo kuimarisha mshikamano uliopo ili kukukuza na kuimarisha demokrasia nchini.

4. Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza akiwasilisha mada kuhusu mambo yanayotakiwa kuzingatiwa na Vyama vya Siasa wakati wa Zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa katika mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa(RPP), Mhe. Jaji, Francis Mutungi na viongozi wakuu wa Vyama vya Siasa nchini leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulihusu kuwapitisha viongozi hao katika hatua zitakazopitiwa wakati zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa. Linalotarajiwa kuanza tarehe 17, Machi 2020.

‘’Tumeamua kukutana na wadau ili kuondoa ombwe kuhusu utekelezaji wa sheria ya Vyama vya siasa ya mwaka 2019, kwani suala la uhakiki lipo kisheria, serikali inatambua changamoto zilizopo katika vyama vya siasa na zoezi hili limekusudia kujenga msingi wa pamoja wa kujitathimini wapi tulipotoka, tulipo na tunapokwenda’’ alisema Jaji Mutungi.

Akifafanua zaidi Jaji Mutungi aliwataka Viongozi wa vyama vya siasa kulitazama zoezi hilo katika taswira chanya kwa kuwa zoezi hilo limekusudia kujenga amani ndani ya vyama hivyo katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika nchini kote mwezi Oktoba mwaka huu.

5. Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party (UDP) akichangia mada wakati wa Mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Mhe .Jaji, Francis Mutungi na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa kuhusu zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (ORPP) inatarajia kufanya zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini kuanzia tarehe 17 Machi, 2020.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba alisema vyama vya siasa havina pingamizi kuhusu zoezi la uhakiki na badala yake aliitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutoa muda wa miezi mitatu ili kuhakikisha kuwa vyama vyote vinakamilisha masuala mbalimbali ya kiutendaji na taratibu zote za msingi kama inavyoelekezwa katika sheria.

6. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi – CUF akichangia mada wakati wa Mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Mhe .Jaji, Francis Mutungi (hayupo pichani) na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa kuhusu zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (ORPP) inatarajia kufanya zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini kuanzia tarehe 17 Machi, 2020.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, vyama vyote vinapaswa kuwa na wanachama wenye uwezo wa kiutendaji ikiwemo kuwa na kadi za uanachama, hivyo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa havina budi kuongeza muda ili kutoa nafasi kwa vyama hivyo kuweza kuhakiki wanachama wake.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda aliitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutengeneza mwongozo wa mfumo wa adili za uongozi ndani ya vyama vya siasa na utaratibu huo uendeshwe katika vikao vya Baraza la Vyama vya siasa nchini.

7. Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Juma Abdullah Saadala akichangia mada wakati wa Mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Mhe .Jaji, Francis Mutungi (hayupo pichani) na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa kuhusu zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (ORPP) inatarajia kufanya zoezi la uhakiki wa Vyama vya Siasa nchini kuanzia tarehe 17 Machi, 2020.

Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya Viongozi wa vyama vya siasa nchini, Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo aliipongeza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa utaratibu wa kufanya vikao kwani utaratibu huo haukuwepo tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini miaka 28 iliyopita.

571 thoughts on “Jaji Mutungi: Zoezi la Uhakiki wa Vyama Halifuti Chama cha Siasa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama